Skip to main content

 


SOMO: KUTAHARAKISHA KWA KUSUDI LA MUNGU

MHUBIRI: Pst, Dr. Eva Mbise  |    09/02/1015

UTANGULIZI:

KUTAHARAKISHWA (QUICKEN), Ni kutokutulia/ kutokuwa na amani. Kunakuwa na nguvu inayokuwa ndani isiyokuacha utulie; kutokea ndani yako na kukulazimisha kufanya mambo.

Nataka kuzungumza kwa Habari ya Nguvu inayokaa ndani yetu inayotakiwa kufanya kazi kwa ajili ya Mungu kwa kile kitu alichoweka ndani ya kila mmoja.

Kila mtu anafahamu kuna kitu kimewekwa ndani cha Ki-Mungu atakama tulizaliwa kwa Bahati mbaya (wengine wanaseema mtoto wa Nyongeza) kwa Mungu hakuna Bahati Mbaya.

Ni kazi ya Roho Mtakatifu tunayempokea kupitia Kristo Yesu kukaa ndani yetu lakini hawezi kunyamaza huku ndani yetu, anataka kitu cha Ki-Mungu kifanyike ndani yetu. Hivyo ni kazi yake kukisukuma hicho kitu kitoke ndani yetu kuja nje ili kutudhihirishia ulichokibeba.

ukikaa na kutulia tu hatuwezi kuona kile ulichobeba. Hivyo Roho Mtakatifu anapokaa ndani yako na kusukuma kile kitu ndani yako ndipo tunaona lile kusudi lililowekwa kwako.

Kipi kinachokutaharakisha?

1.    Ni moja ya kazi ya Roho Mtakatifu anapokuwa ndani yako kukutaharakisha; kukupeleka katika majukumu ambayo MUNGU amekusudia kuweka ndani yako

2.    Ni kazi ya Roho Mtakatifu kutusukuma, kutunyima amani, kutukosesha utulivu mioyoni mwetu ili kutizima azima  nzima ya kuumbwa kwetu.

3.    Roho Mtakatifu anakuwa kichocheo cha kutokutulia ndani yako huku akisukuma kwa mzigo kile ulichoumbiwa kukifanya kutokea nje.

Matendo ya Mitume 9:15 – 16 SUV

15. Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.

16. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.

Huu ni uchaguzi wa mtumishi wa Mungu Paulo zamani akiitwa Sauli. Kipindi akiwa Sauli alitumikia kusudi lakini katika mlango m’mbaya. Kristo akakutana nae na akamgeuza ili atumikie Kusudi lakini katika mlango mzuri.

Anayeambiwa hivi anamjua Paulo, anamjua anafanya nini hvyo anamwambia Mungu huyu hafai katika kazi hii. Lakini MUNGU anamwambia mtu huyu nimemchagua mimi. Nenda muonyeshe yampasayo kufanya.

Tazama ‘15. Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.”

Haleluya!!!

Kwa wakati ule Kristo hakuona mtu mwingine mwenye kusudi aliyeumbwa achukue Jina la Mungu na kupeleka kwa mataifa hofu ilikuwa kwa kanisa. Lakini Paulo kwa sababu aliumbwa kwa wakati ule; hiki ni chombo changu nenda kanitakasie, utakapomtakasa/ mtenge usiache kumwambia yatakayomkuta. Tazama “16. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.”

 

Kwa wito ulioitiwa hakuna tu Raha, hakuna tu Pumziko hata kama kanisa la NENO LA NEEMA wamesema NI MWAKA WA KUTANUKA; inawezekana wenzako wakawa wanatanuka lakini wewe unatanuka katika mateso.

 

Kumbuka Paulo alikuwa mahali anaomba, akaja nabii wa Bwana aitwa Agabo akachukua mkanda wa mtu aitwae Paulo akafunga kiunoni mwake akisema, “ Hivi ninavyo funga huu mkanda, mwenye huu mkanda vipigo vinamsubiri…” Matendo 21:11

Paulo akasema najua KUSUDI nililoitiwa hivyo sitishwi na vipigo vilivyombele maana tangia kuitwa niliambiwa vitisho vilivyombele… nakuambia mtu mmoja anayefikiria kwa Mungu ni mteremko; kwa Mungu ni shwari… Shwari ipo lakini WITO wako unavitu vyake; pale unapopita kwenye mapito MUNGU anataka kujivunia wewe, unapopita anataka kusikia wewe ukisema NIMEMUONA, ANAPONYA, ANAINUA…

 

Ona Agabo anamwambia Paulo unaenda kuonana na haya kesho, lkn Paulo anasema siogopi kuhusiana na hayo hata kama nikufa nipo tayari.

 

Kutaharakishwa na kusudi kwanza, ukubali maumivu, ukubali kupoteza Jina lako, Ukubali watu wakutenge, wakukatae. Hata kama watu/ dunia yote ikatae kukaa na wewe lakini uko tayari kusimama na Mungu bado utasimama.

 

Naongea na Mtu eh! Haleluya…

Kila kusudi lina wito wake ndani. Hatuwezi kupanda UZURI kwenye UBAYA, lazima tung’oe ubaya ili tupande Uzuri.

 

Yeremiah aliitwa kwenye kusudi (Yeremia 1:10).

Kumbuka Paulo aliitwa abebe jina la Kristo kwa Mataifa, Yeremia aliitwa kuwa nabii wa Mataifa na Wafalme. Kutokana wito wake aliishia gerezani.

Lakini hawakuzuia kusudi lake huko  walipomuweka maana kusudi halizuiliki.

 

Kila mtu amebeba kusudi ndani yake na kama hujui inabidi ukae chini ujiulize kwa karibu.

Wagalatia 1:15 -16

Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,

16. alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;

Paulo aipogundua kusudi alijiambia mwenyewe ndani yake Mimi nimeitwa kwa ajili ya hili kusudi lazima niwaambie watu Habari ya Injili ilivyobadilisha maisha yangu. Lengo nikaitoe kwa watu.

 

Roho Mtakatifu nimekwambia kazi yake ni kusukuma hilo kusudi wewe ukijifanya umenyamaza utashangaa unaanza kuota ukihubiri Habari njema za Bwana YESU KRISTO, ukiangalia kioo unaona mataifa ukiyahubiria ‘Njooni kwa Yesu!’ ujue tayari ni msukumo wa Kusudi.

-        Ukiona mtoto  anaanza kuomba na Kubandikia wenzake mikono tambua kwamba kuna kitu klipo ndani unatakiwa kukilea.

-        Ukiona mtoto ameamka na anafuata BIBLIA na kuanza kusoma hata kama hajui kusoma mwachie anapoangalia kuna mambo huishwa ndani yake.
Haleluya!! Nina mtu anakusudi hapa?

 

Waamuzi 13:24 – 25

24. Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, BWANA akambarikia.

25. Roho ya BWANA ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.

“Mbingu inapotafuta kufanya jambo hapa duniani inaangalia tumbo la mtu alietayari na kuweka uzao wenye kusudi hata kwa jambo la miaka 25  mbele”

Kusudi la kuzaliwa kwa Samson lilikuwa Bwana ajilipizie kisasi. Hivyo yeye hakuwa na kuogopa lolote. Kumbuka kusudi haliombwi, kusudi hatulifungii!.Kusudi tunazaliwa nalo,  Kusudi linatokea ndani yetu.

Samson, akavaliwa na kusudi la kulipiza kisasi; akiona watu kunaibuka hasira. Akiona watu wanatesa kanisa la Bwana inalipuka kulipiza kisasi. Sio yeye ni kusudi.
Ukimwangalia mtoto wako unaona nini?

Ukijiangalia unaona nini? Kwa sababu kinachokutaharakisha ni kile unachoona ndani.

 Ukiona upo nyoronyoro sana TAFUTA KUSUDI.

 

Isaya 58:1 – 14

1. Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.

2. Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu.

3. Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

 

Isaya 61:1- 3
1. Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

2. Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;

3. kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.

 

è Hakuna Utukufu katika vitu BALI kuna utukufu katika KUSUDI. Unapolitumikia kusudi, kusudi huachialia Utukufu. Kadri unavyoishi/ Kudumu katika kusudi ndivyo Mungu anavyoachilia UKUU, HESHIMA, UTUKUFU, NAFASI N.K

è Kuna watu leo hawaoni furaha ya WOKOVU, hawaoni maongezeko na kutanuka; yaani wamedumaa na wamekuwa sababu ya kulaumu oh MUNGU hajibu, Mungu hasemi… Upo katika kusudi lipi ambalo leo akija anakukuta mko na Usemi.

Mf. Umeajiriwa mahali (Mkuu wa ofisi na Mwajiriwa) wao huwasiliana mara kwa mara kwa kuonana na kupigiana simu kwa sababu ya uunganiko wa kazi, Vivyo hvyo nasi jatika Ufalme. Mungu huongea sana tu na Marafiki zake.

Matendo 20:22 – 24

22. Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko;

23. isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.

24. Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.

- Nakumbuka tulipokuja mara ya kwanza Kibaga, Kinyerezi (Mahala tulipoweka HEMA la KUKUTANIKIA) mimi na Hefsiba hapakuwa na mazingira mazuri palikuwa kumejaa maji lakini tulipozunguka eneo, tukaambiana hivi “Panatufaa” japokuwa panaonekana pako duni, pamekufa lakini sisi tumejaa uhai tupachukue.

Wenzetu tunawaambiaje hapa, nkamjibu tusiogope na tulipowaambia tuliitikiwa vizuri na kupata hela ya kupachukua na leo unapaona vile kulivyoo sasa nab ado hakujafikia vile viwango tulivyovioona.

Nataka nikutangazie Leo, kwa ajili ya kusudi piga hatua nenda mbele na ujisemeshe kuwa ninaweza, mimi ninamiliki hapa!

Mwenye kusudi HUPISHWA; watu hunyanyuka kwenye viti na kupisha wenye kusudi.

Usiniambie nimezaliwa katika familia duni au nimezaliwa familia isiyofaa; kwa sabubu hiyo siwezi kuwa kile natakiwa kuwa, nitakujibu akili yako ndio imekufa wala akili ya Kristo haipo ndani yako lakini  Mungu huinua akili zilizokufa na kuzipa kufanya kazi upya.

“… Katika kusudi hakuna jambo jepesi”

Yoeli 2:28 -29

28. Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29. tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

 

Matendo ya Mitume 1:8

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

 

2 Timotheo 1:7

7. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

8. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;

- > Wewe una Roho wa Bwana ndani yako, ambaye ana uwezo, Nguvu anainua mambo mapya, haombwi huyu yupo ndani yako.

Kipi kinachokuogopesha?; Kipi kinachokuumiza?. Unae ROHO wa BWANA

 

è Kwa nini tuishi kwenye KUSUDI sasa?

Kuambukiza Tamaduni za Ufalme wa Mungu katika mazingira tunayoishi. Kama vile koloni zilivyotuambukiza taratibu zao vivyo hivyo na tamaduni za ki-Mungu lazima tuziambukize.

(i)               Kuwa na Tabia/Maamuzi na mikao ya KiMungu ktk maisha yetu

(ii)              Kutengeneza watu wenye Tabia za Ufalme wa Mungu mahali tulipo.

(iii)            Kuathiri mikao ya Wana wa Mungu kwa tamaduni za Kifalme

Kuna watu tunaenda Hospitali kutembelea watu/ jamaa / ndugu na marafiki lakini hatuwaambi watu hapo Habari njema.

Kuna watu tunapanda daladala kila siku lakini hatusemi habari za Ufalme wa Mungu

Jiulize na Tafakari kwa kina juu ya KUSUDI LAKO.

Kusikiliza na kutaza fundisho hili kwa youtube 



Umebarikiwa!!!

Kwa mafundisho haya na mengine mengi usisite kutufuatilia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii bofya hapa


Comments