SOMO : KUTAHARAKISHA KWA KUSUDI LA MUNGU MHUBIRI : Pst , Dr. Eva Mbise | 09/02/1015 UTANGULIZI: KUTAHARAKISHWA (QUICKEN), Ni kutokutulia/ kutokuwa na amani. Kunakuwa na nguvu inayokuwa ndani isiyokuacha utulie; kutokea ndani yako na kukulazimisha kufanya mambo. Nataka kuzungumza kwa Habari ya Nguvu inayokaa ndani yetu inayotakiwa kufanya kazi kwa ajili ya Mungu kwa kile kitu alichoweka ndani ya kila mmoja. Kila mtu anafahamu kuna kitu kimewekwa ndani cha Ki-Mungu atakama tulizaliwa kwa Bahati mbaya (wengine wanaseema mtoto wa Nyongeza) kwa Mungu hakuna Bahati Mbaya. Ni kazi ya Roho Mtakatifu tunayempokea kupitia Kristo Yesu kukaa ndani yetu lakini hawezi kunyamaza huku ndani yetu, anataka kitu cha Ki-Mungu kifanyike ndani yetu. Hivyo ni kazi yake kukisukuma hicho kitu kitoke ndani yetu kuja nje ili kutudhihirishia ulichokibeba. ukikaa na kutulia tu hatuwezi kuona kile ulichobeba. Hivyo Roho Mtakatifu anapokaa ndani yako na kusukuma kile kitu...